Wolper Kasahau Maumivu ya Mapenzi

KWELI au anazuga? Mkali wa sinema za Kibongo ambaye amegeukia kwenye ubunifu wa mavazi, Jacqueline Wolper Massawe amesema kuwa sasa hivi amesahau maumivu ya mapenzi.

 

Wolper ameliambia gazeti hili bora la mastaa la Ijumaa kuwa, zamani alikuwa akiumizwa mno kwa sababu alikuwa hajui jinsi ya kulipiza, lakini sasa amejua kila kitu hivyo aachi moyo wake uteseke.

 

“Nimejifunza kitu kimoja, usikubali mtu akuumize. Kama mtu ana-date (anatembea kimapenzi) na rafiki yako na wewe tembea na rafiki yake ngoma iwe droo, hapo kutakuwa hakuna maumivu,” alisema Wolper ambaye alishatendwa na wanaume kibao akiwemo yule jamaa maarufu kwa jina la Mkongo wa Wolper, Harmonize na wengine.

STORI NA IMELDA MTEMA