Penniel Mungilwa ‘Penny’

 

HANA gundu! Mtangazaji wa Kituo cha Magic Swahili kupitia kipindi chake cha Harusini, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amesema tangu alipotengana na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anamshukuru Mungu hajamuachia gundu.

 

Katika mahojiano na Gazeti la Ijumaa, Penny alisema baadhi ya watu wamekuwa wakisema tangu aachane na Diamond au Mondi hajapata tena mwanaume hajawahi kupata mwanaume wa maana.

“Unajua watu wanasema hivyo kwa sababu zamani nilikuwa ninatoka na Diamond ambaye anajulikana. Baada ya hapo nipo na mtu wangu mwingine ambaye hapendi kabisa kujulikana na ninaendelea vizuri tu sasa hao wanaosema nimeachiwa gundu, hawana jipya, mimi niko safi,” alisema Penny.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *